Ripoti ya ABNA- Akizungumza na wanachama wa Umoja wa Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Iran barani Ulaya, Ayatullahil Udhama Ali Khamenei amesema, wanafunzi haswa walioko nje ya nchi wana jukumu la kufikisha ujumbe wa uadilifu na matukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kila pembe ya dunia, ili kuondoa kasumba na propaganda chafu inayoenezwa na vyombo vya habari vya Wamagharibi dhidi ya taifa la Iran. Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, ulimwengu unafaa kufahamishwa kuwa, kumtegemea Allah, kujiamini taifa la Iran na kufuata maagizo na mwelekeo wa kipekee wa Muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ndiyo mambo ya msingi yaliyopelekea kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979. Aidha, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mafaniko yaliyofikiwa na Iran katika nyuga zote na kusema kuwa, madola ya kibeberu yanatiwa kiwewe na maendeleo hayo na hivyo kujaribu kutumia njia za propaganda chafu dhidi ya taifa hili
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 288015
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaasa wanafunzi hususan walioko nje ya nchi kueneza mitazamo na misimamo ya kiadilifu ya Iran.